KUTEKWA KWA MO DEWJI: "BINGO" YA SH. BILIONI 1 YATANGAZWA KWA MTU ATAKAYETOA TAARIFA ZITAKAZOWEZESHA KUPATIKANA KWAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, October 15, 2018

KUTEKWA KWA MO DEWJI: "BINGO" YA SH. BILIONI 1 YATANGAZWA KWA MTU ATAKAYETOA TAARIFA ZITAKAZOWEZESHA KUPATIKANA KWAKE


NA K-VIS BLOG

FAMILIA ya Mohammed Dewji MO, imetangaza zawadi ya shilingi bilioni 1 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo aliyetekwa Oktoba 11, 2018.

Akitangaza “bingo” hiyo mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya kundi la makampuni ya Melt Group jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15, 2018 kwa niaba ya familia ya Bwana na Bibi Gulam Dewji, Msemaji wa familia hiyo Bw. Azim Dewji alisema kwa mtu yeyote mwenye taarifa hizo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Bw. Murtaza Dewji kupitia namba 0755030014 au 0784783228/ 0717208478 au kupitia barua pepe yaani email: findmo@melt.net.

Katika mkutano huo baba wa MO Bw. Gulam Dewji alikuwepo na hawakupokea maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
Bw. Azim Dewji

MO Dewji alitekwa Oktoba 11, 2018 majira ya Alfajiri kati ya saa 11 na saa 11;40 baada ya kushuka kwenye gari lake akielekea kwenye ukumbi wa mazoezi (Gym) kwenye hoteli ya Colosseum iliyoko barabara ya Haile Selasie Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo polisi wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa MO ambaye pia ana hisa za umiliki wa klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Simba kwa asilimia 49, alitekwa na watu wane wawili kati yao wakiwa ni wazungu. Hadi kufikia jana Oktoba 14, 2018, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu 26 wako mikononi mwa polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Taarifa kamili ya familia hii hapa chini.
Loading...

No comments: