LUGOLA AWASILI KATAVI, AWATAKA WAKUU WA IDARA WA MKOA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI HUMO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, October 1, 2018

LUGOLA AWASILI KATAVI, AWATAKA WAKUU WA IDARA WA MKOA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI HUMO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Idara wa Mkoa wa Katavi, alipowasili mjini Mpanda Mkoani humo leo, akitokea Mkoani Kigoma. Lugola aliwataka Wakuu wa Idara hao kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, ACP Damas Nyanda alipokua anafafanua jambo katika Kikao cha Wakuu wa Idara wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoani humo. Watatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdallah Malela. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (kulia) akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), wakati Waziri huyo alipofanya ziara Ofisi za Mkoa huo kwa ajili ya kujua ushirikiano wa watendaji wakuu wa Mkoa huo pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Lilian Matinga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Lilian Matinga (kulia), akimpokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alipowasili katika ofisi za mkoa huo, mjini Mpanda leo, kwa ajili ya kufanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Idara wa Mkoa wa mkoa huo kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wakuu wa Idara hao na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani humo.
Loading...

No comments: