Major Lazer waja na ‘Loyal’, awamu hii wakiwa na Kizz Daniel na Kranium - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, October 4, 2018

Major Lazer waja na ‘Loyal’, awamu hii wakiwa na Kizz Daniel na Kranium


Major Lazer wameachia wimbo mpya, ‘Loyal’ waliomshirikisha staa wa Jamaica,  Kranium pamoja na hitmaker wa Nigeria,  Kizz Daniel, Jumatano hii. Wimbo huu umekuja na video yake, ya nne katika ushirikiano wa Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini,  Adriaan Louw
Tazama video ya Loyal hapa:


‘Loyal’ ni wimbo wa mwisho katika nyimbo za ushirikiano kati ya Major Lazer na wasanii wa Afrika ikifuata baada ya ‘Tied Up’ wakiwashirikisha Mr. Eazi na Raye, “Orkant/Balance Pon It” wakimshirikisha muimbaji wa Afrika Kusini, Babes Wodumo na ‘All My Life’ wakimshirikisha staa wa Nigeria, Burna Boy.
Hivi karibuni Major Lazer waliachia mkusanyiko mpya wa nyimbo wa Afrobeats Mix, unaojumuisha muziki toka bara la Afrika na kuusambaza katika majukwaa yao ya kimataifa.
Bendi hiyo inafanya ziara yake Afrika kuanzia September na October na kupita katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya na Uganda.
Pamoja na ziara ya kimuziki, Major Lazer wameungana na asasi ya VETPAW (Veterans Empowered to Protect African Wildlife) kusaidia kukuza uelewa kuhusu uwindaji haramu barani Afrika.
Wakiwa Afrika, Major Lazer watatembelea makao makuu ya VETPAW kushiriki katika kampeni za kutokomeza uharamia na kujifunza zaidi kuhusu changamoto zake na jinsi ya kubaliana nazo.
Loading...

No comments: