MAKALA; AINA 10 ZA WASAFIRI WA UBER - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, October 25, 2018

MAKALA; AINA 10 ZA WASAFIRI WA UBER

Kampuni ya Uber iliadhimisha miaka 5 barani Afrika hivi majuzi. Hii ni hatua kubwa sana Ikizingatiwa kwamba tulianza kutoa huduma zetu barani Afrika katika jiji la Johannesburg mwaka 2014, Sasa huduma za Uber zinapatikana katika miji mingine kumi na tatu barani Afrika, miji hii ni pamoja na Dar es Salaam, Lagos, Cape Town, Accra, na Nairobi Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Cairo na Aleksandria huko Misri, Afrika Kaskazini.

Wasafiri wanaotumia Uber wamekuwa nguzo muhimu katika kupeleka biashara yetu mebele, tangu tufungue milango yetu barani Afrika. Madereva washirika wengi kutoka kote barani Afrika wanakiri kwamba katika shughuli zao za kila siku wameweza kukutana na wasafiri wa aina mbalimbali - hali ambayo umewafanya wafurahie kutumia app hii ambayo imewasaidia kuwafahamu kutoka tamaduni tofauti tofauti!

Kila Msafiri anayetumia Uber ana sifa zinazomtambulisha kwa namna ya pekee - kwa mfano kuna wasafiri wanaoabiri kiti cha mbele na kufanya mazungumzo ya kufurahisha na dereva, au wasafiri wanaoabiri kiti cha nyuma ili kumalizia kazi fulani wanapokuwa safarini kwenda kwenye mkutano au wale wanaopenda kusikiliza muziki wa sauti kubwa wanapokuwa safarini ..., kila msafiri ana mchango muhimu katika kufanikisha safari za Uber zinazosisimua.


Hawa hapa ni aina 10 ya Wasafiri utakaokutana nao kwenye safari za Uber - wewe ni msafiri wa aina gani?


Anayejua Mitaa Yote

Msafiri wa aina hii hana haja ya kutumia ramani tena, madereva wengi hupenda Wasafiri wa aina hii wa wapandaji. Msafiri wa aina hii anajua michepuko yote ya barabara na hii husaidia sana kunapokuwa na foleni kubwa ya magari kwenye barabara kuud. Ufahamu wao wa barabara na michepuko ya barabara husaidia sana kwa sababu dereva unaweza kutumia barabara tofauti na ukawahi kufikia kwenye mkutano wako wa Jumatatu jijini Dar es Salaam. Ingawa madereva hutumia mfumo wa GPS, inakuwa vizuri sana pale msafiri anapojua barabara ambayo ni fupi na ambayo ukitumia utawahi kufika mahali unakoendai.


Wasafiri Wanaojua Kila Kitu

Baadhi ya wasafiri hupenda kukaa mbele na kujenga muamala mzuri na dereva kwa mazungumzo yao na huzungumzia mambo mengi muhimu. Kama vile migahawa inayouza chakula kizuri jijini Dar es Salaam, au maeneo ambayo kuna fundi magari wazuri wa bei nafuu katika eneo fulani. Msafiri kama huyu ni tunu kubwa kwa sababu ana mengi ya kusimulia kuhusu mtaa husika na hufanya safari iwe ya kusisimua kupitia mazungumzo ya kuchekesha na ana taarifa muhimu sana zinazoweza kukusaidia. Je, kuna mtu ametaja nyota 5?


Msafiri Anayependa Muziki


Baadhi ya wasafiri wanapenda sana kusikiliza muziki wanapokuwa safarini, hasa, wanapenda nyimbo zinazotesa mjini, bila shaka huwezi kumsahau msafiri kama huyu hata kama safari yenyewe ilikuwa fupi. Ima unataka kuweka kitu kipya alichoachilia Diamond Platnumz au Ali Kiba aina hii ya Msafiri anataka awe DJ anapokuwa safarini na mara nyingi huomba keno ya kuunganisha sauti kwenye simu yake. Mara nyingi Msafiri kama huyu anajua kuchagua nyimbo nzuri na dereva hufurahia aina ya muziki anaocheza kiasi kwamba siku yote inakuwa kama wikendi hata kama ni siku ya kawaida tu.

Mjasiriamali
Baadhi ya wasafiri hutumia Uber kujiongeza katika biashara yao. Ima ni kuongeza kituo kingine cha kusimama kwa muda wa dakika 3 ili awasilishe mzigo kwa mteja, au anaongeza kituo kingine cha kusimama ili kuwajulia hali wateja wake, Msafiri kama huyu anafaidi sana kwa kutumia Uber kufanya mizunguko yake mjini. Mzigo umeingia!


Msafiri Mkimya

Baadhi ya wasafiri hupenda kukaa kimya wanapoabiri Uber na mara nyingi hujishughulisha na mambo na hawasemi chochote kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari. Hawataki kusikiliza muziki au kutumia simu zao kuchati au kuperuzi. Mara nyingi Wasafiri wa aina hii hutumia muda wanaokuwa safarini kutafakari na kama njia ya kupumzika - sio kwamba hawana nidhamu au hawapendi watu - kimsingi ni aina ya wasafiri wanaoweza kukaa kimya na kutulia.


Wanaokula Bata

Tanzania ni nchi ambayo viwanja vya starehe huwa "vimechangamka" sana hasa wakati wa usiku, Uwepo wa klabu na kumbi nyingi za starehe unawapa wateja nafasi nyingi ya kuchagua maeneo ambayo wangependa kula bata. Kwa hiyo, kuna aina nyingine ya wasafiri ambao wanakula bata kuanzia mwanzoni mwa safari hadi mwisho. Msafiri kama huyu huwa amepiga pamba kali, amejipodoa kwelikweli na nywele zake zinawaacha watu wengi hoi. Msafiri kama huyu huwa anaenda kula bata maeneo kama vile Havoc au Jozi Lounge na yuko tayari kupiga kumwaga radhi mjini.


Wanaokaa Kiti cha Mbele

Watanzania wanajulikana kwa ukarimu na urafiki, na madereva wengi wanakiri kwamba wasafiri wengi wana muamala mzuri na watu. Wasafiri wa aina hii huwa na mambo mengi ya kuzungumzia, wako tayari kumfahamu dereva na kutaka kumjulia hali yake ya kikexperiences. Siku zote mazungumzo hunogesha safari na kuifanya isiwe ya kuchosha. Hakuna ubaya wowote kujenga urafiki na kuwa mkarimu kwa watu, isitoshe inaboresha tathmini unayopata. Hivi karibuni kampuni ya Uber ilianzisha shindano la wasafiri kutumia kiti cha mbele lililokwenda kwa jina la #Frontseatchallenge shindano ambalo linawahimiza wasafiri kutumia muda wao kuwafahamu madereva zaidi ya kazi yao udereva - kwa nini usishiriki kwenye shindano hili?


Wanaokaa Nyuma Kufanya Kazi Zao

Mara nyingi hawa ni wasafiri waliopiga suti naviatu kali, hutumia muda wao kusoma barua pepe au kupiga simu wanapokuwa njiani kwenda kwenye mkutano au kikao fulani - je umekutana na msafiri wa aina hii? Mara nyingi msafiri wa aina hii huweka mawazo yote kwenye kazi yake yuko bize na kompyuta au simu yake - msafiri kama huyu humtarajia dereva ajue kwamba ana shughuli nyingi na angependa utulivu anapoendelea na kazi yake. Wakati mwingine Msafiri kama huyu ana maarifa mengi ya baishara ambayo humfaidi sana dereva l - kama vile teknolojia mpya iliyoingia mjini, au habari za uwekezaji.


Mtu wa yatu
Maisha ya msafiri wa aina hii yamejaa mambo lukuki - isipokuwa maisha yao ya kijamii yana wigo mpana sana. Atahudhuria Misa ya vijana siku ya Jumapili, sherehe za kuzindua itabu siku ya Jumatatu, ajumuike na wenzake kuimba mashairi siku ya Jumanne, ahudhurie dhifa ya chakula cha jioni kwenye hoteli kubwa, aende kumbi mbalimbali za starehe siku ya Ijumaa - kwa Msafiri wa aina hii, Uber inakuwa kama rafiki wa karibu anayemsaidia katika shughuli zake za maisha ya kila siku.


Wanaobadilisha Maisha ya Wengine

Je, wewe ni msafiri mkarimu mwenye mtazamo chanya wa maisha na angependa kubadilisha maisha ya kila mtu ambaye unakutana naye? Hawa ni wasafiri ambao wamepitia hali ngumu maishani lakini mwishoe wakajikwamua, wasafiri wa aina hii watakupa motisha na kuwa na Jumatatu iliyojaa matumaini. Wasafiri kama hawa watakualika katika ibada katika kanisa lao. Wamejaa chakula cha roho - mtu yeyote akikutana nao anasema tu amen?
Kuna mambo mengo ambayo wasafiri na madereva watarajie hasa idadi ya safari zinapozidi kuongezeka kila wiki. Bila shaka utakutana na wasafiri wenye sifa tofauti tofauti na hili linatupa moyo sana tunapowakutanisha watu mbalimbali!
Loading...

No comments: