Mr Blue aibua shangwe Tigo Fiesta Tanga baada ya kumpandisha Alikiba

Msanii Khery Sameer Rajabu maarufu kama Mr.Blue Jumapili hii alimpandisha msanii Ali Kiba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Mkwakwani mjini  Tanga kwa kushirikiana nae kwenye wimbo wao uitwao MBOGA SABA . Mr Blue alianza kwa kusema “nataka niwape ‘surprise”leo toka kwa ndugu yangu mwenye roho ya pekee aje apande hapa juu awasalimie na niimbe nae,”.

Ndipo Kiba akapanda na kuulipua uwanja  Mkwakwani kwa mayowe, baada ya kumalizika kwa wimbo huo Kiba alisalimia na kushuka jukwaani kitu ambacho mashabiki walitamani aendelee kuimba lakini hakuwa kwenye orodha.
Kwa upande wa wasanii wengine  Rostam na Maua Sama waliendeleza “Remix” yao ya IOKOTE na kuwapa mashabiki Vibe Lote. Nao kundi la Weusi kushirikiana na Nandy waliweza kuimba pamoja na kukonga nyoyo za mashabiki uwanja wa Mkwakwani.
Tamasha la Tigo Fiesta linaambatana na shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tigo Fiesta Supa Nyota na kwa mkoa wa Tanga, msanii Faraji Majimoto aliibuka mshindi atayeiwakilisha mkoa wa Tanga.
Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, wamewaletea wateja wao ofa kabambe ya intaneti wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
Tamasha hilo litaendelea ijumaa hii kwenye uwanja wa Kiruma mkoani Mwanza.

Post a Comment

0 Comments