MWAMNYANGE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM,AWATOA HOFU WANANCHI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 5, 2018

MWAMNYANGE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM,AWATOA HOFU WANANCHI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange akiwa ameongozana mwenyeji wake ,Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja alipofanya ziara ya kutembelea Miradi Mikubwa ya Maji katika jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange akipanda kwenye moja ya Matanki Makubwa ya kuhifadhia Maji katika eneo la Goba kuangalia maenedeleo ya ujenzi wa tanki hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonesha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange maeneo ambayo yatanufaika na huduma ya maji Safi mara baada ya miradi hiyo kukamilika.

Sehemu ya Matengenezo katika mradi huo ukiendelea.
Moja ya Matanki ya kuhifadhia maji ambalo matengenezo yake yanaendelea.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha ramani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange ,maeneo ambayo tayari zoezi la upanuzi wa mtandao wa huduma ya maji unfanyika.
Moja ya eneo la Mradi wa kusukm maji ambao ujenzi wake unaendelea.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange alipotembelea moja ya mradi unaojengwa kwa ajili ya mashine za kusukuma maji .
Moja ya Transfoma zilizofungwa katika Mashine za kusukuma maji kwa ajili ya kuhakikisha umeme una pozwa kabla ya kuingia kwenye mtambo.
Sehemu ya chini ya tenki ambayo hutumika kwa ajili ya kuhifadhi maji kabla ya kwenda kwa watumiaji .
Tenki kubwa la kuhifadhi maji lilipo katika eneo la Kibamba ambalo tayari limeanza kufanya kazi ka sasa.


Anaandika  Dixon Busagaga,Dar es Salaam .

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Jenerali  Mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi ,Davis Mwamnyange amewatoa hofu wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Pwani juu ya upatikanaji wa huduma ya Maji .

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea  miradi mikubwa ya Majisafi kwa ajili ya kujionea maendeleo ya miradi hiyo ,Jenerali Mwamnyange amesema kukamilika kwa mradi huo kwa kiasi kikubwa kutapunguza adha ya maji kwa baadhi ya maeneo kama si kumaliza kabisa tatizo la maji .

Miongoni mwa maneo ya mradi aliyotembelea ni pamoja na mfumo wa Maji uliopo Bunju,mfumo wa maji Salasala,mfumo wa maji Makongo na Changanyikeni  pamoja na kutembelea Matanki ya kuhifadhia Maji katika maeneo ya Madale ,Goba na Kibamba.

Jenerali Mwamnyange akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi ,DAWASA ,Mhandisi Gaudence Aksante pamoja na mwenyeji wao ,Afisa mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja ameonesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huku akiwataka Wakandarasi kukamilisha miradi hiyo kama walivyokubaliana.

“Ziara hii imekuwa fursa nzuri sana kwangu kama mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA,nimeweza kujionea mwenyewe hali halisi ya mradi huu  itakaoongeza huduma ya Maji katika jiji la Dar es Salaam “alisema Jenerali Mwamnyange.

“Hatua iliyofikiwa ni nzuri ,inatia moyo na wananchi wawe na matumaini makubwa kwamba sasa huduma ya maji itakua bora zaidi baada ya kukamilika kwa mradi huu,Kasi ya Wakandarasi sasa hivi wanajitahidi baada ya hatua kuchukuliwa na Mamlaka kuwahimiza pamoja na serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji”aliongeza Jenerali Mwamnyange .

Alisema licha ya changamoto walizoeleza awali zilizochangia kupungua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo tayari matatizo yale yametatuliwa  na sasa wanaendelea vizuri na kwamba kwa kasi iliyopo wataweza kumaliza mradi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa upande wake Afusa Mtendaji Mkuu ,Dawasa,Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza huduma ya upatikanaji wa maji ambapo watu Milioni moja wanataraji kufikiwa na huduma.

Alisema mradi huo ukianza hali ya mivujo ya maji iliyopo kwa baadhi ya maeneo itapungua kwa sababu maji yataenda kwa watu na kwamba awali tatizo lililokuwepo ni kwamba maji yalikuwa ni mengi lakini mtandao wa maji ni mdogo kwa sasa matumizi yataongezeka.

“ Tatizo la wizi wa maji nalo pia tunatarajia kuisha ,kwa sababu wizi wa maji ulikuwepo kutokana na kukosekana kwa maji ,lakini sasa huduma ya maji ipo na tayari tumeanza kuwananishia wananchi maji kwa mkopo hivyo wajitokeze tu kuomba kuunganishiwa huduma ya maji.”alisema Mhandisi Luhemeja.

Mwisho.
Loading...

No comments: