NAIBU MKURUGENZI MKUU UNEP ATEMBELEA SEKONDARI YA JANGWANI ATAKA WASICHANA KUJIPANGA KUWANIA NAFASI ZA JUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 19, 2018

NAIBU MKURUGENZI MKUU UNEP ATEMBELEA SEKONDARI YA JANGWANI ATAKA WASICHANA KUJIPANGA KUWANIA NAFASI ZA JUU

 
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Bi. Nyaibuli Boke (wa pili kushoto), Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani (kulia) katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (wa pili kulia) aliyeambatana na Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya (kushoto) alipofanya ziara fupi ya kutembelea shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam. 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani kuwamasisha kufanya vyema kwenye masomo yao alipotembelea shuleni hapo kuwashukuru walimu kwani bila wao asingefika hapo wakati wa ziara yake nchini jana jijini Dar es Salaam.

 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani kuwamasisha kufanya vyema kwenye masomo yao alipotembelea shuleni hapo kuwashukuru walimu kwani bila wao asingefika hapo wakati wa ziara yake nchini jana jijini Dar es Salaam.

 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya katika picha ya pamoja na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani mara baada ya kuwahamasisha na kuwatia moyo wakati wa ziara yake fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.

 
Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) kuhusu UNEP inavyoshirikiana na Wizara ya Elimu kuandaa mwongozo wa ufundishaji mazingira katika shule ili wanafunzi waenzi na kuthamini mazingira tangu wakiwa wadogo wakati wa ziara ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (kushoto) shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na vyombo vya habari kuhusu ziara yake shule ya Sekondari Jangwani  ya kutia hamasa kwa wasichana wa shule hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya
 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na kubadilishana mawazo na Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Bi. Nyaibuli Boke (katikati) pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani (kushoto) mara baada ya kuwasili shuleni hapo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo jana jijini Dar es Salaam.

 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akisaini kitabu cha wageni cha Shule ya Sekondari Jangwani mara baada ya kuwasili shuleni hapo kutia hamasa kwa wasichana wa shule hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani.

 
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (hayupo pichani) alipokuwa akiwapa hamasa ya kufanya vyema kwenye masomo yao ikiwemo na kujitambua wakati wa ziara fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.


Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Bi. Nyaibuli Boke (wa pili kushoto) na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani wakiongozana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (wa pili kulia) aliyeambatana na Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya (kulia) kuelekea kwenye eneo maalum la kuzungumza na wasichana wa shule hiyo jana jijini Dar es Salaam.
 
NA MWANDISHI WETU
NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya amewataka wasichana nchini kujipanga vyema kutafuta maisha kwa kuzingatia fursa ambazo zipo. Akizungumza baada ya kutembelea shule ya sekondari Jangwani ambayo na yeye alisoma katika miaka ya 1970 Mkurugenzi huyo alisema elimu ni mojawapo ya kitu muhimu katika kufanikisha malengo ya kuwa juu kiuchumi na kimadaraka. Alisema nafasi za juu zinaweza kupatikana kwa kukazania elimu, kujituma kwa bidii na kujifunza kutoka kwa wengine hasa nchi zilizoendelea. Alisema wakati yeye anasoma hapakuwepo na nafasi kubwa kwa wasichana lakini kwa sasa nafasi zipo wazi na wakijipanga vyema watakuwa miongoni mwa watu wanaoendesha uchumi na kutegemewa na familia zao. Alisema kitu muhimu kwa wasichana waliopo sasa ni kujijenga kwa namna ambavyo wataweza kutumika vyema katika sekta zozote huku wakiendeleza uhusiano mzuri na familia zao ambazo ndio msingi wa mafanikio. Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya ziara yake hiyo ya kutia hamasa wasichana wa Jangwani alisema mazingira magumu yaliyoelezwa na Mkuu wa shule ya sekondari Jangwani  ataangalia namna ya kusaidia ingawa si moja kwa moja kulingana na nafasi yake. Katika mazungumzo Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 1,470 , mwalimu Bi. Nyaibuli Boke alisema shulehiyo inakabiliwa na changamoto za mabweni kwani lililopo linakidhi mahitaji ya walemavu kwa asilimia 75 huku asilimia zilizobaki ni za wanafunzi wa kawaida. Aidha alisema wana uhaba wa vitabu vya mchepuo wa Sanaa a na pia zana za walemavu za kujifunzia zikiwa pungufu. Pamoja na changamoto zilizopo ambazo zilisababisha shule hiyo kushuka ufaulu, mwalimu Boke ambaye amehamishiwa hapo mwaka huu akitoka sekondari ya King’ongo iliyopo manispaa ya Ubungo, alisema wamejipanga kurejesha heshima ya shule hiyo. Alisema kumekuwa na kamati ya mitihani, kurejesha hamu ya ufaulu na pia kuwa na mazungumzo na wazazi kwa wale wanafunzi ambao wanaonekana hawafanyi vyema kujua matatizo na kusaidia kuyatatua. Alisema wamekuwa wakishirikisha wazazi kufanikisha kampeni ya kuzingatia kauli mbiu ya divisheni ziro na 4 mwiko. Katika mazungumzo yake na wasichana Naibu Mkurugenzi huyo aliwataka kujidhatiti katika masomo na kutambua nafasi zao kwa kuwa wazi kujifunza. Alisema amerejea nchini baada ya kuteuliwa nafasi yake kuangalia nini ambacho anaweza kusaidia akiwa kiongozi wa mazingira katika masuala ya mazingira. Akijibu swali kuhusu mradi wa kufua umeme wa Stiglers gorge Naibu huyo alisema kwamba hana shaka na juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutunza mazingira kwa kuwa ofisi ya Tanzania ya UNEP inafanyakazi karibu sana na serikali katika suala la mazingira kupitia Ofisi ya Makamu wa rais, Baraza La Mazingira na taasisi nyingine kama Wizara ya Elimu. Alisema pamoja na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali anatumia ziara yake hiyo kushauriana kuhusiana na masuala ya mazingira na nini ambacho UNEP inaweza kuisaidia serikali katika jukumu la utunzaji wa mazingira. Alisema kimataifa Tanzania inajulikana kwa kuwa na mbuga za wanyama na bahari hivyo iko katika nafasi nzuri ya kujulikana na anachofanya kama Naibu ni kujua wapi wanaweza kusaidia. “Tanzania ni tajiri sana katika mambo ya mazingira ukisema Tanzania watu wanafikiria mbuga za wanyama wanafikiria bahari. Kwa nje Tanzania iko vizuri “ alisema. Naye Clara Makenya Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini ambaye alikuwa katika ziara ya naibu huyo alisema kwamba UNEP imeshirikiana na Wizara ya Elimu kuandaa mwongozo wa ufundishaji mazingira katika shule ili wanafunzi waenzi na kuthamini mazingira tangu wakiwa wadogo.
 
Loading...

No comments: