RAIS MAGUFULI ACHUKIZWA NA KIWANGO DUNI CHA TIMU YA TAIFA STARS - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 19, 2018

RAIS MAGUFULI ACHUKIZWA NA KIWANGO DUNI CHA TIMU YA TAIFA STARSRais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania –Taifa stars kuelekea mchezo wa 5 wa kundi L unaotarajiwa kupigwa November 18 Mjini Maseru nchini Lesotho.

Akizungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Magufuli ametoa fedha hizo kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi na kuongeza morali ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo huo Muhimu dhidi ya Lesotho.

Aidha Rais Magufuli ameonesha kukerwa kwakwe na kufanya vibaya kwa timu hiyo ya Taifa na vilabu mbalimbali vya hapa nchini hasa katika michuano ya kimataifa.

Akizungumza katika hafla hiyo Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars Erasto Nyoni na Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike wameahidi kufanya vyema katika michezo miwili iliyosalia katika kundi L.

Awali waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na Rais wa TFF Wallace Karia wamezungumzia mipango ya kuivusha timu hiyo kwa ajili ya michuano ya AFCON mwakani nchini Cameroon.

Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi L la michuano ya kufuzu kwa fainali za AFCON zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon, nyuma ya Uganda The Cranes inayoongoza kundi hilo.

Na Amos Nyanduku.... ACN

Loading...

No comments: