Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lafana Songea (Picha) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, October 15, 2018

Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lafana Songea (Picha)


Likiwa limeingia mkoa wanne Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote limefana na kuacha alama kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma usiku wa kuamkia jana, Kabla ya kuingia mkoani humo Tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro limepita mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea na kuelekea Mtwara jumapili hii.
Msanii wa muziki wa hip hip Zaid akionyesha makeke yake mbele.
Akifungua Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololite Mgema alisema Tunawashukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kutuletea tamasha hili kubwa mkoani kwetu.
“Hii si kwa burudani pekee bali ni fursa kwa wakaazi wa mkoa huu kwa kuwawezesha kwa kuwaongezea kipato kwa kipindi hiki chote cha wiki nzima .Niendelee kuwapongeza tena Tigo na Clouds Media na kuwaomba mwakani msiache kuja tena kwenye mkoa wetu.
Nyomi ya wakazi wa Songea
Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumpata mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota kwa kumuibua Msanii Single Baba atakayeiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar Es Salaam mwezi ujao.
Shoo rasmi ilianza kwa Msanii Mesen Selekta kufuatiwa na Rubby huyu ni msanii aliyeibuliwa kwenye Nyota miaka kadhaa iliyopita, kwa kweli ni msanii wa aina yake aliweza kuteka hisia za mashabiki kwa kuimba nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze,Ntade, Na Yule,Forever na nyingine.
Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme
Jumla ya wasanii kumi na mbili walipanda jukwaani wakiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba,Zayd, Fid Q, Masen Selekta, Lulu Diva,Chege, Foby ambao wasanii hao ndio watapanda kwenye jukwaa jumapili uwanja wa Nangw’anda Mtwara.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.
Lulu Diva akiwasha moto.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim,Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
Mesen Selekta
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Loading...

No comments: