Ngoma
ya Kabila la wamaasai wakiimba katika Tamasha la Urithi Festival
lililozinduliwa Jijini Arusha Katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid .Picha
na Vero Ignatus.
Baadhi
ya washiriki wakila ugali wa asili na mlenda katika tamasha la urithi
festival katika uwanja wa shekh Amri Abeid Jijini Arusha na Vero
Ignatus.
Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa mkoani Arusha. Picha na Vero Ignatus
Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akiwa katika moja ya banda wanalotengeneza vitu vya asili. Picha na Vero Ignatus.
Kutoka katikati ni Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi, kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ambaye pia ni Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha la Urithi, akifuatiwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega. (Picha na Vero Ignatus).
Kushoto
ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audix Mabula, Katibu Mkuu
wizara ya habari michezo michezo na Utamaduni Suzan Mlawi wakiwa katika
moja ya banda uwanjani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Ngoma ya asili ya Wakina mama kutoka kabila la Kimeru. Picha na Vero Ignatus
Hawa
nao wakinamama kutoka kabila la Kimaasai walipamba Tamasha hilo la
Urithi na utamaduni mkoani Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid.
Picha na Vero Ignatus.
Na Vero Ignatus, Arusha
Kila
mwaka mkoa unatakiwa kutenga fungu kwaajili ya kuandaa tamasha la
urithi na utamaduni itakayochangia kuzaa zao jipya la utalii na kupanua
wigo wa vivutio vya utalii nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi
katika uzinduzi wa Tamasha la Urithi lililozinduliwa Jijini Arusha
katika uwanja wa Shekh Amri Abeid na kushirikisha makabila mbalimbali
mkoani hapo. Ameeleza
kuwa Taifa lisilo na utamaduni ni taifa lililokufa, sambamba na
kupoteza rasilimaliza husika kwani utamaduni ni kuvutio kibwa cha
utalii.
"Tusipoenzi
na kuzitunza tamaduni hizo utu wetu rasilimali zetu zitapotea, kwani
utamaduni wetu ni kivutio kikubwa cha utalii"alisema Katibu Suzan
Kwa upande wake Katibu tawala wa
Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema asilima 80%wageni wanaoingia nchini wanatembelea Mkoani hapo kutokana na vivutio vilivyopo mkoani Arusha kupitia vya utalii
Maonyesho
hayo yamehusisha wadau kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula
vya asili,mavazi ya asili ,utalii na tamaduni za Mtanzania bila kuvunja
sheria .
Tutapata
nafasi nzuri za kuona tamaduni mbalimbali za kuona mambo mbalimbali,
mavazi, vyakula, michezo ya asili, alisema Kwitega.
Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula
ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kubuni wazo hilo zuri,
kwa kutambua na kuthani, kutafiti na kuhifadhi vitu vya asili kwa
manufaa ya Watanzania na kwa vizazi vijavyo.
Ikumbukwe
kuwa septemba 15 Tamasha la Urithi Festival lilizinduliwa rasmi Jijini
Dodoma na Makamu wa Rais Samia Suluhu likiwa na kauli mbiu isemayo
"Urithi wetu Fahari yetu"
Maonyesho
hayo yamehusisha wadau mbalimbali kuonyesha mambo burudani,ngoma za
asili,vyakula vya asili,mavazazi ya asili ,utalii na tamaduni
Kuhifadhi tamaduni zetu nzuri
Tamasha hilo la urithi litafungwa tarehe 13 octoba na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanjawa Shekh Amri Abeid Arusha.
No comments:
Post a Comment