Tigo yaadhimisha kwa aina yake wiki ya huduma kwa wateja - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, October 4, 2018

Tigo yaadhimisha kwa aina yake wiki ya huduma kwa wateja
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa (kati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo wafanyakazi wa Tigo waliwatembelea wateja mitaani na kukusanya maoni yao kuhusu huduma zake. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja .


Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo wafanyakazi wa Tigo waliwatembelea wateja mitaani na kukusanya maoni yao kuhusu huduma zake. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja.


Msaidizi wa Huduma za Tigo, Plasidia Jameson (kati) pamoja na Msaidizi wa Ubora wa Huduma za Tigo, Kejiya Thangal (kulia) wakielezea baadhi ya huduma za Tigo kwa mfanyabiashara wa soko la Mwenge, Dismas Msauthi (kushoto), hii ikiwa kwa nia ya kuboresha utoaji huduma kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Tigo, Wilfred Nestory (kushoto) akielezea baadhi ya huduma za Tigo kwa wafanyabiashara wa soko la Mwenge, Joseph Luseba (kulia)  na Samuel Gervas (kati), hii ikiwa kwa nia ya kuboresha utoaji huduma kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Kiongozi wa Timu wa Huduma kwa Wateja ya Tigo, Jackson Jerry (kulia) pamoja na Meneja Mauzo wa Tigo – Kinondoni Aznat Mboya (aliyesimama kati) – Kinondoni, Aznat Mboya (kushoto) wakikusanya maoni na kuelezea baadhi ya huduma za Tigo kwa Elizabeth Simon wa Mwenge Dar es Salaam kwa nia ya kuboresha utoaji huduma, hii ikiwa kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Meneja Mauzo wa Tigo – Kinondoni, Asnat Mboya (kushoto) akikusanya maoni na kuelezea baadhi ya huduma za Tigo kwa Juma Ibrahim mkaazi wa Mlalakuwa na Mohammed Sultan wa Manzese Dar es Salaam kwa nia ya kuboresha utoaji huduma, hii ikiwa kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
a

Loading...

No comments: