DK Mwakyembe atoa Tuzo za Habari za Maji kwa mwandishi mahiri juu ya Uwajibikaji katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 5, 2018

DK Mwakyembe atoa Tuzo za Habari za Maji kwa mwandishi mahiri juu ya Uwajibikaji katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji
Shirika la Shahidi wa Maji kupitia programu ya Uhakika wa Maji kwa kushirikiana na Shirika la Water Witness International, WaterAid pamoja na Journalist Environmental Association of Tanzania (JET), waliandaa shindano la kuwania Tuzo kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari. Tuzo hizi zinajulikana kama Tuzo za Habari za Maji kwa waandishi mahiri wa masuala ya Uwajibikaji kuhusu Usimamizi wa Rasilimali za Maji. Mpango huu ulibuniwa ikiwa ni sehemu ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa rasilimali za maji katika kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda, utalii, afya na uvuvi. Vilevile kuongeza uwajibikaji wa jamii na taasisi zinazohusika katika sekta ya maji. Shindano la Tuzo hizi lilizinduliwa rasmi mwezi Juni 2017 katika warsha ya mafunzo iliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Usimamizi wa rasilimali za maji.

Malengo ya Tuzo za Habari za maji
Shindano la “Tuzo ya Habari za Maji” lilikuwa na malengo yafuatayo:  
  1. Kutambua na kuthamini mchango muhimu wa waandishi wa habari katika kuelimisha na kupelekea utatuzi wa changamoto za usimamizi wa rasilimali za maji nchini na;
  2. Kuongeza uelewa wa vyombo vya habari na jamii kuhusu masuala ya maji.
Kwa kutambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya maji na kuwajibisha wahusika katika Serikali na mashirika binafsi, tumeona umuhimu wa kukuza vipaji vya waandishi wa habari katika kuelimisha na kuboresha juhudi za Usimamizi wa Rasilimali za maji. Shindano la mwaka 2017/2018 la Tuzo za Habari za Maji lilikua na makundi yafuatayo:
  1. Mwandishi Bora wa habari aliyetumia taarifa za Mradi wa Uhakika wa Maji
  2. Uandishi bora wa kiasili kwa Uhakika wa Maji (Best original journalism for a water security)
  3. Mwandishi Bora wa habari za maji mwenye umri mdogo.
  4. Chombo Bora cha habari kuripoti kuhusu masuala ya maji.

Idadi ya Wanahabari walioshi kushindania tuzo
Jumla ya washiriki ilikua 47 ambapo kazi zilizowasilishwa zilikua ni zaidi ya 120.

Mchakato wa kuchagua washindi
Timu ya majaji wenye fani na uzoezu mkubwa katika masuala ya maji, mazingira na habari walifanya mapitio ya kazi zote zilizotumwa na kuchagua washindi kutokana na vigezo vilivyowekwa. Kazi hii ilifanyika kwa mahiri mkubwa pasipo kuwa na upendeleo.


M Majina ya Washindi katika kila kundi na zawadi walizopata ni kama ifuatavyo:
  1. Sylvester Domasa amejishindia zawadi ya kombe la tuzo, kompyuta mpakato aina ya aina ya Hewlett Packard Pavilion 360 na fedha kiasi cha TZS 500,000/=
  2. Nuzulack Dausen amejishindia zawadi ya kombe la tuzo,kompyuta mpakato aina ya aina ya Hewlett Packard Pavilion 360 na fedha kiasi cha TZS 500,000/=
  3. Amina Semagogwa amejishindia zawadi ya kombe la tuzo, HP Chromebook 11 na kamera aina ya Sony DSCH300 Compact Bridge

Kutangazwa kwa awamu nyingine ya shindano la tuzo za Habari za Maji
Tuzo hizi zitaendelea kwa kipindi kingine cha miaka miwili chini ya Shirika la Shahidi wa Maji na lakini inakusudiwa kuwa endelevu kwa kushirikiana na wizara ya Maji, Wizara ya Habari na wadau wengine. Tangazo la Shindano lijalo litatolewa kupitia vyombo vya habari na mitandao mwazoni mwa mwaka 2019. Tunatarajia kuongeza wigo mpana wa tuzo zitakazoshindaniwa.

Loading...

No comments: