JESHI LA POLISI LIMETOA TAARIFA ZA AWALI ZA KUTEKWA KWA MO DEWJI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 19, 2018

JESHI LA POLISI LIMETOA TAARIFA ZA AWALI ZA KUTEKWA KWA MO DEWJI


Wakati juhudi za kumtafuta mohamed Dewji zinaendelea Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa mbali na vitendo  viovu vinavyoendelea kujitotokeza hali ya sasa ni shwari ukilinganisha na mwezi januali mwaka jana.

Akielezea oparesheni zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na wizi wa magari,ujambazi,na tukio lililo jitokeza mapema wiki iliyopita la kutekwa kwa Mohamed Dewji na kusema kuwa baada ya tukio kufanyika walibahatika kupata risasi mbili ambazo bado zinaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Aidha IGP Sirro amesema kuwa kwa kutumia cctv camera ametaja aina ya gari ambayo ilitumika kumteka MO pamoja na njia mbazo walitumia kupita baada ya kufanya tukio hilo la utekaji ambapo kwa kuendelea kufuatilia tukio hilo imegudulika kuwa gari hilo limetokea nchi jilani.

siro amesema jeshi kwa kushirikiana na wanachi wameendelea kupata taarifa nyingi zinazosaidia kurahisisha upatikanaji wa mo dewij na kutoa rai kwa wanchi wenye uwezo wa kuwa na silaha,na wenye uwezo wa kifedha ni vyema kuwa na silaha zao ambazo zinaweza kuwa msaada kutokana na hali ya sasa kubadilika.

MO amefikisha siku ya nane tangu kutekwa kwake huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi na kutoa taarifa za awali
Na.. Amos Nyanduku... ACN
Loading...

No comments: