WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO UTAKAPOJENGWA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA STIEGLERS GORGE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, October 5, 2018

WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO UTAKAPOJENGWA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA STIEGLERS GORGE Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo lililoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa  Kuzalisha Umeme katika  Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge wakati alipotembelea eneo hilo Oktoba 4, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akizungumza baada ya kutembelea eneo  la ujenzi wa Mradi wa  Umeme wa Moporomoko ya  Mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA,  Fuad Abdallah wakati alipotembelea Stesheni ya TAZARA ya Fuga kukagua ujenzi wa tawi la reli hiyo  litalounganisha steheni hiyo na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo wakati alipowasili kwenye  eneo utakapojengwa  Mradi wa  Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji  - Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na wapili kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika  reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa  Mradi wa Umeme wa Maporomoko  ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge  wakati alipotembelea eno hilo Oktoba 4, 2018.  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na  eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea Stesheni hiyo, Oktoba 4, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Eneo litakapojengwa tuta la kukinga maji  katika  Mradi wa Kuzalisha Umeme kwenye  Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge  ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitembelea, Oktoba 4, 2018
Loading...

No comments: