Afya ya Mugabe Yazidi Kuwa Mbaya ..Hawezi Kutembea - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, November 25, 2018

Afya ya Mugabe Yazidi Kuwa Mbaya ..Hawezi Kutembea

MUGABE

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa amekiambia chama cha ZANU-PF kuwa baba wa Taifa hilo Rober Mugabe kuwa sasa hawezi kutembea na yuko nchini Singapore kwa matibabu.

Rais Mnangagwa ametoa taarifa hiyo jana Novemba 24 alipokuwa akihutubia mkutano huko Murombedzi, ambako alikuwa wakipita kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura.

Kwa mujibu wa Rais Mnangagwa, Robert Mugabe alikuwa kwenye nchi hiyo ya bara la Asia kwa zaidi ya miezi miwili akipatiwa matibabu, lakini hivi karibuni hali yake imekuwa mbaya zaidi kutokana na umri wake, hivyo kupelekea kushindwa kutembea.

Kutokana na hilo Rais Mnangagwa amesema kwamba kama taifa litafanya chochote anachotaka afanyiwe, kwani ni jukumu lao kumuangalia.

“Sasa hivi ni mzee sana, sasa hivi hawezi kutembea lakini kwa chochote atakachotaka tutatoa, tunamuangalia, yeye ni Baba wa Taifa hili la Zimbabwe, ni baba wa Taifa huru la Zimbabwe”, alinukuliwa Emerson Mnangagwa akiwaambai wana ZANU-PF na vyombo vya habari vilivyokuwepo maeneo hayo.

Robert Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka 94 ndiye mtu aliyelipatia taifa hilo uhuru akishirikiana na viongozi wengine wa Afrika kama Mwl. Nyerere wa Tanzania, na alikaa madarakani kwa miaka 37 mpaka pale alipojiuzulu baada ya jeshi kumtaka afanye hivyo.
Loading...

No comments: