Balaa lingine latangazwa kwa watumiaji wa Instagram - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, November 21, 2018

Balaa lingine latangazwa kwa watumiaji wa Instagram


Kwa watumiaji wa mtandao wa Instagram ambao wanatumia Apps za kupata likes na followers feki kwenye akaunti zao, kwa sasa ujanja huo hautakuwepo tena kwani mtandao huo umeanzisha kampeni ya kufuta likes na followers wote ambao ni bandia.
Image result for instagram fake followers and likes
Sheria hiyo mpya ambayo imeanza kutumika tayari na mtandao huo, itatumia mfumo wa Machine Learning ambao utaondoa followers na likes zote feki, pamoja na komenti ambazo zimetoka nje ya mfumo wa kawaida wa mtandao huo.
Mabadiliko hayo huenda ya kawa tishio kwa akaunti ambazo zinafanya biashara ya matangazo kwenye mtandao huo, kwani wengi wamekuwa wakiwahadaa wateja wao kuwa kurasa zao zinatembelewa na watu wengi kwa kuwaonesha likes, comments na followers wao na hata impression ya akaunti zao.
Hili ni balaa la pili kufanyika kwenye mtandao wa Instagram, baada ya mwanzoni mwa mwaka huu kutangaza kufuta akaunti zote feki kwenye mtandao huo.

Loading...

No comments: