BALOZI WA PALESTINA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 29, 2018

BALOZI WA PALESTINA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)


 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akielezea namna wagonjwa wa moyo wanavyofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na kupatiwa matibabu ya karibu katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa balozi wa Palestina nchini  Mhe. Hamdi Mansour AbuAli alipotembelea chumba cha ICU wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

 
Mkuu wa huduma za Sheria na Katibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maulid Kikondo akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kutembelea ukarabati wa wodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

 
Mkuu wa huduma za Sheria na Katibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maulid Kikondo akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kutembelea ukarabati wa wodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

 
Baba wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua Hamis Daud akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya mtoto wake baada ya kufanyiwa upasuaji huo alipofanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kutembelea wagonjwa wodini leo Jijini Dar es Salaam

 
Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli akizungumza na menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ambavyo Palestina itashirikiana na taasisi hiyo katika masuala mbalimbali ya afya ya moyo baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA GENOFEVA MATEMU – JKCI)
Loading...

No comments: