Bobi Wine Amwaga machozi Kuzama kwa boti ziwa Victoria, apoteza marafiki zake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, November 25, 2018

Bobi Wine Amwaga machozi Kuzama kwa boti ziwa Victoria, apoteza marafiki zake


UGANDA, BOBI WINE, AJALI YA BOTI
Mbunge wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda,  Robert Kyagulanyi maarufu ‘Bobi Wine
Kampala, Uganda. Mbunge wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda,  Robert Kyagulanyi maarufu ‘Bobi Wine’ amesema baadhi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya boti iliyotokea katika ziwa Victoria ni watu wake wa karibu.
Mwanamuziki huyo amesema amesikitishwa na tukio hilo na kusisitiza amewatuma wasaidizi wake kupeleka boti kwa ajili ya kusaidia kazi ya uokoaji.
“Bado siwezi kuamini tumepoteza vijana wengi. Moyo wangu unaumia. Nimepoteza marafiki wangu kadhaa na inaumiza sana. Tunaendelea kuziombea familia za waliopoteza wapendwa wao na wale waliojeruhiwa tunawaombea wapone haraka,” amesema.
AJALI ,UGANDA
Inakadiriwa watu wapatao 30 wamefariki dunia na zaidi ya 60 wanahofiwa kuwa wamezama baada ya boti kuzama katika upande wa Uganda wa Ziwa Victoria.
Kulingana na taarifa za maofisa wa polisi wa Uganda, boti hiyo iliyokuwa imebeba mamia ya abiria ilizama kutokana na hali mbaya ya hewa jana Jumamosi.
Mkurugenzi wa shughuli kwa polisi wa Uganda amesema, miili 29 imeopolewa majini na watu wengine 26 wameokolewa.

No comments: