Dkt Abbasi Awataka Waandishi kufuata Sheria ya Habari - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, November 21, 2018

Dkt Abbasi Awataka Waandishi kufuata Sheria ya Habari

Na Grace Semfuko-MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amewataka waandishi wa habari kutumia haki na wajibu wao katika kulinda maadili yao ya uandishi na kutotumia taaluma yao kukejeli na kuchafua watu wengine

Amesema Sheria mpya namba 12 ya mwaka 2016 ya huduma za vyombo vya habari kifungu cha 7 ingawa inawapa Waandishi wa Habari kukusanya,kuhariri na kusambaza habari lakini haiwapi fursa waandishi hao kuandika habari ambazo zinachafua wengine.

Dkt Abbasi aliyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha Hallow Tanzania kinachorushwa na Radio Uhuru ya Jijini Dar Es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali Nchini.

“Sheria Mpya ya Habari inawapa fursa Waandishi kufanya kazi zao za kukusanya,kuhariri na kusambaza habari,sheria hii haijamnyima Mwandishi wa Habari kupata habari, lakini pia haijatoa fursa za kusambaza habari za kukejeli na kuchafua wengine, sheria itachukua nafasi yake kwa atakaebainika kufanya hivyo” alisema Dkt Hassan Abbasi Msemaji Mkuu wa Serikali.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Magufuli kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni sehemu ya kulinda maadili ya uandishi wa habari na kuvitaka vyombo vingine kuendelea kuheshimu,kulinda na kutetea maslahi ya Taifa.

Akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Aggrey Manzi kuhusiana na baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii katika kuchafua wengine, Dkt Abbasi alisema sio sahihi kutumia mitandao hiyo katika kuona wengine hawafai, bali mitandao itumike kutangaza habari za Maendeleo.

Loading...

No comments: