FORBES IMETOA TAKWIMU YA WASANII WA KIKE WALIOINGIZA MKWANJA MREFU 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, November 21, 2018

FORBES IMETOA TAKWIMU YA WASANII WA KIKE WALIOINGIZA MKWANJA MREFU 2018


November 20 Jarida maarufu la biashara nchini Marekani la Forbes Limetoa List kamili ya wasanii wa kike Duniani walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2018.
Mwanadada Katy Perry anayefanya muziki aina ya Pop amefanikiwa kukamata nafasi ya kwanza akiwa anaingiza kiasi cha Dola Million 83 ikitokana na Ziara yake ya muziki ya Witness,muziki pamoja na Dili alizosaini.
Taylor Swift anayefanya muziki wa Pop pia amefanikiwa kukamata nafasi ya akiingiza kiasi cha Dola Million 80,ikitokana na mauzo makubwa ya album yake ya Reputation, Ziara ya muziki pamoja na Dili alizosaini.
Mwaka jana Beyonce alikuwa anaongoza kwa kuingiza kiasi cha Dola Million 105 lakini mwaka huu ameshuka mpaka nafasi ya 3 kwa kuingiza kiasi cha Dola million 60.
ORODHA YA KUMI BORA
1Katy Perry ($83 million)
2. Taylor Swift ($80 million)
3. Beyoncé ($60 million)
4. Pink ($52 million)
5. Lady Gaga ($50 million)
6. Jennifer Lopez ($47 million)
7. Rihanna ($37.5 million)
8. Helene Fischer ($32 million)
9. Celine Dion ($31 million)
10. Britney Spears ($30 million)

Loading...

No comments: