Freeman Mbowe, Ester Matiko Warudishwa Gereani....Ni Baada Ya Serikali Kukata Rufaa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, November 30, 2018

Freeman Mbowe, Ester Matiko Warudishwa Gereani....Ni Baada Ya Serikali Kukata Rufaa


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesimamisha kwa muda mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko hadi rufaa iliyofunguliwa na jamhuri katika Mahakama ya Rufaa utakapotolewa.

Mbowe na Matiko, walifungua maombi ya pingamizi kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwafutia dhamana kwa kukiuka masharti.

Jana, upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka maombi hayo yatupwe kutoka na kukiuka baadhi ya sheria katika maombi yao hata hivyo Jaji Sam Rumanyika alitupilia mbali ombi hilo na kusikiliza shauri hilo.

Akisoma uamuzi huo mahakamani hapo leo Ijumaa Novemba 30, Jaji Rumanyika, amesema upande wa jamhuri ulifungua maombi ya kupinga uamuzi wa Jaji Rumanyika wa kupinga  usikilizaji wa hatua ya rufaa.

Alisema sheria inampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufungua maombi ya kupata rufaa wakati shauri likiendelea kwa ngazi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.

“Mahakama Kuu imesimamisha mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na upande wa utetezi wakipinga uamuzi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuwafutia dhamana, kesi hiyo itaendelea baada ya Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi,” amesema Jaji Rumanyika.
Loading...

No comments: