Hii ndiyo rekodi ya Amunike ndani ya Taifa Stars na mambo 10 muhimu usiyofahamu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, November 19, 2018

Hii ndiyo rekodi ya Amunike ndani ya Taifa Stars na mambo 10 muhimu usiyofahamu

Shirikisho la soka nchini, TFF Agosti 6 mwaka huu lilimtambulisha aliyekuwa mchezaji wa taifa wa Nigeria, Emmanuel Amunike kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars.
Amunike ambaye ni winga wazamani wa klabu ya Barcelona ametua Stars akirithi mikoba ya Salum Mayanga.
Stars chini ya Amunike imeshuhudiwa ikikubali kipigo cha bao 1 – 0 dhidi ya Lesotho matokeo ambayo yamewanyong’onyesha Watanzania katika kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya Afcon hapo mwakani yatakayofanyika Cameroon kufuatia kuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele.
Rekodi ya Emmanuel Amunike tangu kukakibidhiwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ mwezi wa Agosti mwaka huu.
Katika mechi yake ya kwanza Amunike alifanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana 0 – 0 dhidi ya Uganda maarufu kama The Cranes ambao walikuwa nyumbani.
Stars iliyopo kundi ‘L’ chini ya Mnigeria huyo ilijikuta ikipata kipigo cha mabao  3 – 0 mbele ya Cape Verde ugenini.
Amunike akiwa na vijana wake wa Stars kwenye dimba la taifa aliweza kufuta uteja kwa Cape Verde ya kufungwa na badala yake akafanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli 2 – 0 na kufufua matumaini kwa Watanzania safari ya michuano ya Afcon nchini Cameroon mwaka 2019.
Wakati Watanzania wakifikiria ushindi dhidi ya Lesotho ugenini na Waganda hapa nyumbani ambao unaweza kusema ‘wameishatusua’ baada ya kuongoza kundi hilo la ‘L’ wakiwa na alama zao 13, Stars ikajikuta inapokea kipigo cha bao 1 – 0 dhidi ya timu hiyo mchezo uliyopigwa hapo jana siku ya Jumapili.
Mchezaji huyo wazamani wa Nigeria ‘Super Eagle’, Emmanuel Amunike toka aichukue Stars mpaka sasa amefungwa michezo miwili ya Cape Verde na Lesotho, sare moja dhidi ya Uganda huku akifanikiwa kukiongoza kikosi cha Stars kupata ushindi mbele ya Cape Verde nyumbani.
Msimamo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ndani ya kundi ‘L’ kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Afcon itakayofanyika Cameroon mwakani 2019.
Mambo machache usiyoyajua kuhusu kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike
1. Alikuwa akicheza nafasi ya Winga.
2. Amunike ameitumikia Super Eagles kuanzia mwaka 1993 hadi 2001, akicheza mara 27 akifunga magoli 9.
3. Amewahi kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 1994 akiwa na timu ya taifa ya Nigeria
4. Mwaka 1994 Amunike amefunga mabao mawili ambayo yaliisaidia Nigeria kushinda Mataifa ya Afrika fainali iliyofanyika Tunisia.
5. Amunike pia medali ya Olympic akiwa na Nigeria chini ya miaka 23 huko Atlanta mwaka 1996.
6. Ngazi ya klabu amewahi kucheza baadhi ya timu za Ureno, akiitumikia Sporting michezo 51 akishinda mabao 17.
7. Amewahi kushinda mataji ya ligi akiwa na baadhi ya klabu za Nigeria na Misri akiichezea, Julius Berger F.C. na Zamalek SC.
8. Amunike pia amewahi kucheza Hispania kwenye kllabu ya Barcelona kuanzia mwaka 1996 hadi 2000.
9. Amewahi kusaka vipaji kwa Manchester United.
10. Amewahi kupata mafunzo ya uwalimu wa soka na kukiongoza kikosi cha vijana wa chini ya miaka 17 ‘U-17’ cha Nigeria  kombe la dunia huko Chile. Amewahi kuifundisha, Sdanese club Al Khartoum SC Novemba mwaka 2017 na kuachana nayo Machi mwaka 2018.


CHANZO; BONGO5.COM
Loading...

No comments: