Hivi ndio vigezo vya kuwapata wagombea CCM 2020


Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akilakiwa na wajumbe alipowasili ukumbini kuogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
Morogoro. Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimesema kupatikana kwa wagombea wa udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutatokana na ushiriki wao katika shughuli za maendeleo ya chama hicho.
Pia, kimesema hadhi wanayopata wabunge ambao baadhi yao huteuliwa kuwa mawaziri au naibu waziri na madiwani wakiwa wenyeviti wa halmashauri au mameya inatokana na heshima ya CCM kukubalika kwa wananchi.
Hayo yalielezwa jana Jumamosi Novemba 24, 2018 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Karogelesi alipokuwa akifunga mafunzo ya siasa, itikadi na maadili kwa vijana wa chama hicho Kilosa mkoani humo.
Karogelesi alisema chama ndicho kinachowapa tiketi wanachama wake kugombea ubunge na udiwani hivyo wanapochaguliwa hawapaswi kujiweka mbali na shughuli za ujenzi wa CCM.
Alisema hakuna mwanafunzi anayeweza kujivunia kufanikiwa kwake kielimu ikiwa hawezi kutambua au kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na walimu wake ama katika masomo ya awali au shule ya msingi.
"Ili tuwapitishe wagombea wetu kwenye udiwani au ubunge mwaka 2020, tutampima kila mgombea kutokana na ushiriki wake katika kazi za chama bila kumtazama usoni.”
“Sifa ya msingi na ya awali nje ya uanachama wake ni kujihusisha kwake na maendeleo ya CCM," alisema Karogelesi.
Mwenyekiti huyo alisema chama cha siasa kitakachokosa kujijenga, kuimarika na kukubalika hakitapata madiwani na wabunge hivyo hata rais atashindwa kuteua mawaziri na naibu wake.
Alisema kwenye majiji na halmashauri hakutakuwa na wenyeviti au mameya wa CCM.
Aliwataka wabunge wa kuchaguliwa, madiwani na wale wa viti maalumu kutambua kufika kwao walipo sasa kumetokana na nguvu ya chama na si uwezo wao binafsi.


SOMA ZAIDI HAPA BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments