Je wajua kunywa mkojo ni tiba ya magonjwa mbali mbali ;Soma Hapa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, November 26, 2018

Je wajua kunywa mkojo ni tiba ya magonjwa mbali mbali ;Soma Hapa


Mtu kufikia hatua ya kunywa mkojo wake mwenyewe ni jambo ambalo anaweza kulifanya kama amekwama mlimani au jangwani na hana chakula chochote.

Lakini siku hizi baadhi ya watu wameanza kunywa mikojo yao wakiwa majumbani kwao tu.
Kwa mfano Kayleigh Oakley mwenye umri wa miaka 33, ambaye ni mwalimu wa yoga kutoka Newington, anadai kwamba anakunywa mkojo wake mwenyewe kwa sababu umemsaidia kupona baadhi ya maradhi ambayo yalikuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Kayleigh aliwaambia waandishi wa habari kwamba alianza kunywa mkojo wake mwenyewe miaka miwili iliyopita.

"Nilisikia kwamba mkojo unaweza kusaidia kuweka upya mfumo wa kinga, kumfanya mtu kuwa na afya njema na ngozi iwe na muonekano mzuri", alisema mwalimu huyo wa yoga.
Na kwa sasa hanywi tu jagi lililojaa mkojo wake kila siku, lakini pia huwa anajipakaza usoni kwa madai kuwa anatunza ngozi yake. 

Kinachoshangaza zaidi, sio Kayleigh peke yake ambaye anasifia matumizi yake ya mkojo kwa siku za hivi karibuni.

Wiki iliyopita Leah Sampson, mwanamke mwenye miaka 46 kutoka Alberta, Canada aliliambia gazeti la The Sun kuwa kunywa mkojo wake mwenyewe kumemsaidia kupunguza nusu ya uzito wa mwili wake.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Loading...

No comments: