Kampuni ya IPP Limited yatangaza kutengeneza magari nchini Tanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, November 20, 2018

Kampuni ya IPP Limited yatangaza kutengeneza magari nchini Tanzania

Kiwanda cha IPP Automobile Limited kwa kushirikiana na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation (KOTA) kinatarajia kuunda magari aina ya Kia, Hyundai na Daewoo.
Kwa Mujibu wa Azam, Zaidi ya billioni 22 za Kitanzania zimetengwa kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kujengwa Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya hatua ya awali ya kutiliana saini ya makubaliano ya ubia kati ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Automobile Limited, Dkt.
Reginald Mengi na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Thomas Choi . Kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kati ya Septemba na Oktoba mwaka 2019, Tanzania itaanza kutumia gari la kwanza litakaloundwa hapa nchini.
Loading...

No comments: