Manji 'Out' Yanga, orodha kamili wagombea hii hapa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, November 20, 2018

Manji 'Out' Yanga, orodha kamili wagombea hii hapa


Wakati mchujo wa wagombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Yanga ukipangwa kufanyika Ijumaa hii, wagombea 27 wamejitosa kugombea nafasi mbali mbali kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Januari 13.
Tofauti na ilivyotarajiwa, aliyekuwa Mwenyekiti Yusuf Manji, hajachukua wala kuchukuliwa fomu kama ambavyo kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitaka Yanga wafanye endapo watahitaji kumrejesha Manji.


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Ally Mchungahela amesema mchakato wa uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa na tayari zoezi la kuchukua na kurejesha fomu limefungwa na kinachofuata sasa ni mchujo kwa wagombea zoezi litakalofanyika Ijumaa.
Hadi zoezi la kuchukua na kurejesha fomu linafungwa Jumatatu jioni, wagombea 27 walijitokeza huku wanne kati yao wakiwania nafasi ya mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Manji ambaye aliomba kujiuzulu mwaka jana, lakini Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini, George Mkuchika hivi karibuni alitangaza Mwenyekiti yupo na atakuwepo ofisini  rasmi Januari 15.


Mwanasheria wa TFF, Herman Kidifu ameiambia MCL Digital kuwa wagombea waliojitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga.
Kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Kevela wakati wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.
Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geofrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Justine
Peter Bisangwa.Habari kwa hisani ya MWANANCHI

Loading...

No comments: