MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAPEWA SIKU 14 ZAIDI KUWASILISHA TAARIFA ZA MIRADI NA MATUMIZI YA FEDHA ZA MWAKA 2016 NA 2017 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 1, 2018

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAPEWA SIKU 14 ZAIDI KUWASILISHA TAARIFA ZA MIRADI NA MATUMIZI YA FEDHA ZA MWAKA 2016 NA 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto( Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) Dkt. John Jingu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu nyongeza ya siku 14 zaidi zilizotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) wakifuatilia tamko la Katibu Mkuu Dkt. John Jingu la kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW. 
Katibu Mkuu wa Braza la NGOs nchini Bw. Ismail A. Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na kanuni mpya za NGOs (2018) ambazo zimezingatia matakwa ya kanuni za maadili katika kuboresha utendaji wa NGOs wakati wa kikao cha Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii kilichoeleza kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika hayo kuwasilisha taarifa za miradi na fedha kwa Msajili wa NGOs. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW. 


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku kumi nne zaidi (14) kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 zilizokaguliwa kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. 

Tamko hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Ufafanuzi ulitolewa kuwa, “Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alikutana na wawakilishi wa vyombo vya habari na kutoa maagizo yakuyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taalifa zao kwa Mashirika hayo ikiwa ni pamoja na taarifa za miradi na taarifa za fedha zilizo kaguliwa kwa mwaka 2017 na 2018”, alibainisha DKT. Jingu.

Dkt Jingu amefafanua kuwa, maagizo hayo yalipaswa kutekelezwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe 28.9.2018 ya agizo lilipotolewa na Serikali. Hata hivyo imeelezwa kuwa mwitikio wa utekelezaji umekuwa wa kuridhisha kutokana na ukweli kuwa Mashirika mengi yamezingatia maelekezo ya Serikali.
Loading...

No comments: