MBABANE WATUMIWA UJUMBE MZITO NA SIMBA


Kuelekea katika mchezo wao wa jumatano dhidi ya Mbabane Swallow FC ya Swaziland wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa taifa, Simba wameahidi makubwa kwa mashabiki.


Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ni kipenzi cha mashabiki amesema maandalizi yapo vizuri kwa kuwa wamekuwa wakipewa mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya waweze kupata matokeo katika mchezo huo.

"Tupo vizuri wachezaji wote na tunatambua kuwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa, tunaomba Mungu tuweze kupata matokeo kwa kuwa hayo ndio malengo yetu kuweza kushinda mchezo wetu wa kimataifa.


"Jumatano tutakuwa uwanjani, mashabiki wajitokeze kwa wingi maana wana umuhimu sana katika kufanikisha ushindi, watanzania kwa pamoja watupe sapoti katika mashindano haya ya kimataifa hatutawaagusha," alisema Mkude.


Mbabane FC wanatarajiwa kutua leo kwa ajili ya mchezo huo wakiwa chini ya kocha wao wa muda kutoka Malawi ambaye aliwahi kuinoa Mbeya City, Kinah Phiri.

Post a Comment

0 Comments