MCHANA NYAVU HUYU KUIBUKIA YANGA, AFUNGUKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, November 21, 2018

MCHANA NYAVU HUYU KUIBUKIA YANGA, AFUNGUKAMshambuliaji wa timu ya Mbeya City, Eliud Ambokile amesema kuwa yupo tayari kuichezea timu ya Yanga kwa kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo ila amewapa kazi ya kufanya viongozi wa Yanga.


Ambokile anaongoza kwa kutupia ndani ya Ligi Kuu akiwa amefunga mabao 8 mpaka sasa hali iliyofanya Yanga wavutiwe na uwezo wake ili kumsajili.


"Nimewaelekeza viongozi wa Yanga kwamba wakaribie Mbeya ambako ndipo yalipo makao makuu yetu ili wazungumze na viongozi wangu.


"Sina tatizo na kucheza Yanga kikubwa ni makubaliano kwa kuwa kwa sasa bado nina mkataba na timu yangu hivyo sitaweza kujiunga na timu kinyemela," alisema.


Yanga wanatafuta mshambuliaji ambaye atasaidiana na Herieter Makambo na Amiss Tambwe ili kuongeza nguvu katika safu hiyo ambayo bado haijatengamaa kwa mujibu wa kocha mkuu Mwinyi Zahera.


CHANZO; SALEHE JEMBE
Loading...

No comments: