MCHEZAJI MPYA WA SIMBA KUTOKA IVORY COAST AFANYIWA VIPIMO VYA AFYA YA MOYO KABLA YA KUANZA "KAZI" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, November 30, 2018

MCHEZAJI MPYA WA SIMBA KUTOKA IVORY COAST AFANYIWA VIPIMO VYA AFYA YA MOYO KABLA YA KUANZA "KAZI"Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa katika picha ya pamoja na beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar baada ya kuwasili katika taasisi hiyo akiwa na daktari wa timu ya Simba Yassin Gembe kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiliwa na klabu hiyo kupitia dirisha dogo jana Jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akimfanyia beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipowasili katika taasisi hiyo kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana Jijini Dar es Salaam.
 
Fundi Sanifu wa Moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saada Salum akimwekea kifaa cha kupima kiwango cha afya ya moyo ili kuhimili mchezo awapo uwanjani beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam


Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akiangalia mapigo ya moyo na umeme wa moyo unavyofanya kazi katika mashine ya Trade Mill alipokua akimpima beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo.
Loading...

No comments: