MHE HASUNGA AFANYA KIKAO KIZITO NA TIMU YA WATAALAMU OPARESHENI KOROSHO MKOANI MTWARA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 29, 2018

MHE HASUNGA AFANYA KIKAO KIZITO NA TIMU YA WATAALAMU OPARESHENI KOROSHO MKOANI MTWARA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiongoza kikao kazi cha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo Leo tarehe 28 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao kazi cha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo Leo tarehe 28 Novemba 2018.
Kikao kikiendelea
Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo, Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Leo tarehe 28 Novemba 2018 amezuru Mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Katika ziara hiyo Mhe Hasunga atafatilia mwenendo wa ununuzi wa Korosho za wakulima katika kuhakikisha maelekezo ya serikali yanatekelezwa.
Mara baada ya kuwasili Mkoani humo Mhe Hasunga amekutana na wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na kufanya kikao kizito kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo.

Loading...

No comments: