NDEGE MPYA YA TANZANIA AIRBUS 220 YATAMBULISHWA RASMI (PICHA) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, November 24, 2018

NDEGE MPYA YA TANZANIA AIRBUS 220 YATAMBULISHWA RASMI (PICHA)


Kampuni ya uundaji wa ndege ya Airbus huko Mirabel, Montreal nchini Canada, jana iliitambulisha rasmi ndege mpya mali ya mteja wake ambaye ni serikali ya #Tanzania aina ya Airbus A220-300.


Kampuni hiyo imesema kuwa ndege hiyo, itakuwa ndege ya kwanza ya aina hiyo kwa kampuni za ndege barani Afrika.


Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria hadi 160, na ina urefu wa mita 38.7, ina kimo cha urefu wa mita 11. 5 na urefu wa mabawa yake ni mita 35.1. Mbali na hayo, ndege hiyo ina uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 5,920, na pia ina uwezo wa kuwekwa mafuta lita 21,918.


Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ndege hiyo imeundwa katika mfumo wa kumwezesha abiria kusafiri pasi na karaha, kutokana na kuwepo kwa siti pana zinazomfanya abiria kujisikia huru.


Ndege za familia ya Airbus A220 awali zilikuwa zikifahamika kama Bombardier CSeries (au C Series) kwani zilibuniwa na kampuni ya Canada ya Bombardier Aerospace.


Oktoba 2017, kampuni ya Airbus ilinunua umiliki wa asilimia 50.01 wa ndege za CSeries (sasa hivi A220), ambapo Bombardier ilisalia na asilimia 31, huku  Investissement Québec ikiwa na asilimia 19.


A220-300 ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama CS300 iliruka kwa mara ya kwanza 27 Februari 2015, na kupewa cheti cha kwanza tarehe 11 Julai 2016, na ilianza kutoa huduma ikifanya kazi na Shirika la Ndege la Baltic Disemba 14, 2016. Baada ya kuanza kutoa huduma, watu abiria pamoja na marubani wa ndege hiyo walitoa mrejesho, na kuridhishwa na ubora wake pamoja na utendaji kazi.Loading...

No comments: