NIKK WA PILI AANDIKA UJUMBE MZITO KWA RUGE


Rapa wa Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’, amefunguka mengi kuhusiana na mambo aliyofanyiwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumfikisha hapo alipo leo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikk ameandika ujumbe ambao ameuita My story na Ruge Mutahaba unaosomeka;

Muda wa kipindi kirefu sana katika maisha yangu ya shule nilikuwa naamini mim ni mtu wa kukaa nyuma, nisiye na uwezo wa kuzungumza mbele za watu, sikuwa nanyoosha mkono darasani hata kama najua jibu, nilio soma nao chuo wanajua nilivyo kuwa natoroka presentations.

Siku moja niliongea dakika mbili mbele ya watu, akaniona mtu anaitwa Ruge Mutahaba, jioni akaniita tukaaka tukapiga story, baada ya kama lisaa la kupiga story akaniambia, wewe unauwezo mkubwa wa kupanga mawazo, kujenga hoja lakini pia kueleza jambo kirahisi na kuumba taswira.

Akaniambia wewe ni public speaker mzuri, akaanza kunipa nafasi ya kuzungumza mbele za watu nilikuwa naona na kosea lakini kila niliposhuka alikuwa anaiambia umefanya vizuri sana ongeza hichi na hichi.

Leo nimekuwa naalikwa vyuoni, kwenye makongamano, semina,taasisi, kampeni mpaka makanisani, kama mzungumzaji au mtoa mada, na hata mitandaoni huwa naandika mawazo yangu bila woga, ingekuwaje nisingekutana na Ruge Mutahaba.

Mungu akupe wepesi urudi katika uzima wako, RG (genius).

Ruge yupo nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya figo ambayo yanamsumbua kwa miezi kadhaa sasa. Mwenyezi Mungu amjalie apone haraka.

Post a Comment

0 Comments