Pogba awaambia wachezaji wa Juve mpango wake wa kuachana na Man United mwezi Januari - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, November 20, 2018

Pogba awaambia wachezaji wa Juve mpango wake wa kuachana na Man United mwezi Januari

Huwenda klabu ya Juventus ikaendelea na mipango yake ya kutafuta saini ya Paul Pogba dirisha lijalo la usajili la mwezi Januari baada ya nyota huyo wa Manchester United kutangaza kurejea Serie A.
Paul Pogba pictured arriving at Manchester United's training base on Tuesday morning 
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia, Pogba aliwaambia wachezaji wa Juventus kuwa anajiandaa kujiunga na klabu hiyo wakati alipokutananao kwenye mchezo wa Champions League waliyoibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1.
Gazeti la michezo la Corriere dello Sport kutoka nchini Italia limeripoti kuwa vinara hao wa Serie A, Juventus huwenda wakafanikisha dili la kumnasa kiungo huyo wa Ufaransa, Pogba mapema hapo mwakani.
Pogba received a warm reception from Juventus fans at the Allianz Stadium earlier this month
Kwa upande mwingine Juventus haina uhakika ni lini atarejea nyota wao raia wa Ujerumani, Emre Can kutoka katika majeraha aliyokuwa nayo yaliompelekea kufanya upasuaji.
Hata hivyo wanaamini kuwa kiungo huyo wa Ujerumani atarejea katikati ya mwezi Desemba lakini haina uhakika kuhusiana na utimamu wake.
Pogba had the vice-captaincy taken off of him by United manager Jose Mourinho
Akizungumza sababu za kukosekana kwa Pogba mechi dhidi ya Manchester City, Mourinho amesema kuwa Paul anasumbuliwa na majerahabaada ya mechi yao jijini Turin.
Licha ya maneno hayo ya Mourinho, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 wiki hii ameonekana katika starehe huko Dubai, akiwa sambamba na Lionel Messi .
Loading...

No comments: