Polisi wafanya upekuzi nyumbani kwa Zitto - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 1, 2018

Polisi wafanya upekuzi nyumbani kwa Zitto


By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni limefanya upekuzi nyumbani kwa Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.

Jebra Kambole, wakili wa mbunge huyo wa Kigoma Mjini amelieleza Mwananchi leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 kuwa upekuzi huo umefanyika Masaki jijini hapa, nyumbani kwa mbunge huyo.

Jana saa tatu asubuhi Zitto alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake na kupeleka katika Kituo cha polisi Oysterbay ambako alihojiwa kwa saa tatu na kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi.

Kambole amesema baada ya mteja wake kupelekwa kituo kikuu cha polisi, hakulala hapo alihamishiwa kituo kingine kilichopo Mburahati ambako aliondolewa leo asubuhi na kurudishwa kituo cha polisi Oysterbay.
Loading...

No comments: