SERIKALI YASAINI MKATABA WA MKOPO NAFUU WA SHILINGI BILIONI 440.703 PAMOJA NA MSAADA WA SH. BILIONI 45 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 15, 2018

SERIKALI YASAINI MKATABA WA MKOPO NAFUU WA SHILINGI BILIONI 440.703 PAMOJA NA MSAADA WA SH. BILIONI 45 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB)


 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akiwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru wakisaini mikataba ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 ambapo fedha hizo zote zitatumika katika Mradi mkubwa wa umeme mkoani Kigoma, Bajeti Kuu ya Serikali, Kilimo pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo.

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James akisaini moja ya Mikataba hiyo ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 kutoka AfDB katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa wa Hazina jijini Dar es Salaam.

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akizungumza na wanahabari (hawaonekani)pichani mara baada ya kusaini Mikataba hiyo ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa wa Hazina jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru.(PICHA NA MPIGA PICHA WETU).
Loading...

No comments: