TIMU HIZI HAPA SITA HAZIJAPOTEZA, MATOLA WA LIPULI AFUNGUKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, November 24, 2018

TIMU HIZI HAPA SITA HAZIJAPOTEZA, MATOLA WA LIPULI AFUNGUKALigi kuu inaendelea baada ya kusimama kwa muda kupisha mechi za kimataifa, ila mpaka sasa kuna timu sita ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja zikiwa katika uwanja wa nyumbani.

Timu hizo ni pamoja na Yanga, Simba, Azam FC, Mbeya City, Coastal Union na Mtibwa Sugar, na kati ya hizo ni timu moja tu iliyopanda daraja msimu huu ambayo ni Coastal Union.

Timu mbili za Yanga na Azam FC mpaka sasa hazijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kuishia kupata sare katika michezo yao ambayo wamecheza.

Kocha wa Lipuli FC, Seleman Matola alisema kuwa hali hiyo inatokana na kila kikosi kujipanga kuibuka na ushindi licha ya kuwa na ukata kwa kuwa hakuna mdhamini mkuu ndani ya ligi.
Loading...

No comments: