UJERUMANI,UINGEREZA WAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA 100 KUMALIZIKA VITA YA KWANZA YA DUNIA, DAR - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, November 12, 2018

UJERUMANI,UINGEREZA WAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA 100 KUMALIZIKA VITA YA KWANZA YA DUNIA, DAR


 Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiwakilisha Serikali ya Tanzania, akizungumza katika tukio hilo.

 Balozi wa Ujerumani, nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter  akizunumza
 Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akizungumza katika tukio hilo la kumbukumbu ya miaka 100 ya vita kuu ya kwanza ya dunia
Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiwakilisha Serikali ya Tanzania, akizungumza katika tukio hilo.(PICHA NA ANDREW CHALE).
 
Na Andrew Chale, Dar
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa pamoja na Nchi ya Uingereza kupitia Balozi zao hapa nchini leo Novemba 11,2018 wameazimisha kumbukumbu ya miaka 100  tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya Dunia kwa kufanya ibada maalum na kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyopo  eneo la Makumbusho-Kijitonyama,  Jijini Dar e Salaam.
Awali akizungumza katika  tukio hilo,  Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiwakilisha Serikali ya Tanzania, amesema wakati wa vita kuu ya kwanza ya Dunia vinapiganwa,  Tanzania Bara, Rwanda na Burundi ilikuwa nchi moja Koloni la Ujerumani la Afrika Mashariki ambapo licha ya vita hiyo kuisha huko nchi za Ulaya, vita hivyo viliendelea kwa siku kadhaa na askari wa kiafrika walipigana kwa ushujaa mkubwa sana pamoja na askari wa Ujerumani.
“Askari wa kiafrika walipigana kwa ushujaa mkubwa sana pamoja na askari wa Wajerumani ambao hapa baadhi yao wamezikwa na wengine wamezikwa maeno mengine. Katika siku hii ya leo ambapo tunakumbuka askari hao pamoja na askari wengi wa kiafrika, ambao walifarikik dunia wakati huo na pia nchi hii (Tanzania) ambao baada ya vita ilipata madhara makubwa na kuwa ndio nchi ambayo ilisahaulika, nchi ambayo haikupewa maendeleo wala kipaumbele wakati huo.
Leo ni taifa huru lenye kujiamini na kusimama imara. Kwa hiyo siku ya leo hii wote tukumbuke vita sio jambo zuri, bali amani ndio kitu cha msingi katika kuleta maendeleo ya watu wote, sisi Tanzania  tunahistoria ya kujua madhara ya vita, hiyo vita kuu ya kwanza ya dunia, vita kuu ya pili ya dunia, lakini hata tulipoachokozwa na Iddi Amini, kwa hiyo sisi ni taifa linalojua nini madhara ya vita hivyo leo tusisitize amani, tusisitize upendo watanzania wote tuwakumbuke mababu zetu ambao walikufa na hawakuzikwa mahali pa heshima kama hapa, lakini Mungu hawarehemu, awaweke salama mahala pote walipotawanyika na wasipoonekana, Nashukuru” amesema Profesa Kabudi.
Aidha, Profesa Kabudi amewataka watu wasiohitakia mema Tanzania kwa sasa kuacha mara moja kwani Taifa bado lipo imara chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.
“Tuache ubinafsi. Tuache siasa za pesa, tuache kucheleweshana katika maendeleo. Tupeane  nafasi tuitendee haki nchi hii kwa kuipa maendeleo katika miundombinu, katika nishati, katika kilimo, katika afya na nyoote mumeona jana hatua ambazo Mheshimiwa Rais amezichukua kwa kuwaweka askari wetu tayari kwenda kukusanya korosho baada ya kuona kuna  kila dalili ya hujma.
Taifa hili kama mlivyoona  kutoka vita kuu ya kwanza, ya pili, vita vya Uganda, taifa ambalo daima wakati wakati wa shida, daima  wakati wa matatizo linasimama pamoja na jeshi letu  ni jeshi ambalo halijawahi kushindwa  vita hata moja, na vita hivi itavishinda pia, vita vya kiuchumi.” Amemalizia Profesa Kabudi.
Kwa upande wake, Balozi wa Ujerumani, nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter  ameweza kuombea askari hao huku akiwataka raia waliobaki kuendelea kuwakumbuka kwani walipigana katika ukombozi wa kila mmoja wetu aliye hai sasa.
Aidha, mbali na kuweka mashada ya maua katika makaburi hayo, pia zoezi kama hilo kwa viongozi hao Balozi wa Ujerumani, Balozi wa Uingereza na Profesa Kabudi pamoja na  wageni wengine wameweza kuweka pia katika eneo la mnara wa Askari uliopo katikati ya Jiji la Dar Es Salaam.
Pia katika tukio hilo, Mabalozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, taasisi na makampuni na familia za ndugu na jamaa wameweza kujumuika pamoja katika kuweka mashada ya maua ya kumbukumbu pamoja na kufanya ibada maalum.
Vita kuu hiyo ya kwanza askari mbalimbali walipigana wakiwemo wa Ujerumani, Uingereza, India, Ubelgiji na nchi zingine wakiwemo wa Afrika walipigana katika vita hiyo huku na kuzikwa kwenye makaburi mbalimbali ikiwemo hayo ya Jumuiya ya Madola ambayo pia wamezikwa wapiganaji wa Vita ya I na ya II ya Dunia.
Loading...

No comments: