UONGOZI WA SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA SARE NA LIPULI FC - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, November 23, 2018

UONGOZI WA SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA SARE NA LIPULI FC


Baada ya Simba kupata sare ya kutofungana na timu ya Lipuli FC, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Taifa, uongozi umefunguka mipango yao ijayo.

Simba wametoka sare mchezo wao wa 3 wakiwa wameshinda michezo 8 na kupoteza mchezo mmoja kati ya 12 waliyocheza.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema hayo ni matokeo ya mpira hivyo akili zao ni kwenye maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa wa Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika.

"Huu ni mpira na haya ni matokeo, hivyo hakuna namna. sasa nguvu zetu tunazielekeza katika mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows FC ya kutoka Swaziland, utakaochezwa jumatano," alisema.

Matokeo hayo yanawafanya wavune pointi moja uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya pointi 27 wakiachwa na Yanga ambao jana walishinda mbele ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga na kufikisha pointi 29.


KWA HISANI YA SALEHE JEMBE
Loading...

No comments: