VIDEO: Shetta arejea kwenye game kwa kishindo, aachia ngoma mpya ‘Hatufanani’ amshirikisha Jux na Mr. Blue - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, November 30, 2018

VIDEO: Shetta arejea kwenye game kwa kishindo, aachia ngoma mpya ‘Hatufanani’ amshirikisha Jux na Mr. Blue

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Shetta ameachia ngoma yake mpya ‘HATUFANANI’, hii ni baada ya kukaa kimya kwa takribani ya miezi 11 bila kuachia kazi mpya.Kwenye ngoma hiyo amemshirikisha Jux na Mr. Blue, muunganiko ambao umeufanya wimbo upenye vizuri zaidi kwenye masikio pindi unapousikiliza.
Mdundo wa Hatufanani umetengenezwa na Kimamba  Records, na kama ukisiliza kwa haraka haraka biti ya wimbo huu unaweza kuifananisha na wimbo wa Aibu wa Nandy ambao nao umepitia mikononi mwa Kimamba.
Akiongea na Bongo5 kuhusu kimya chake cha muda mrefu kwenye game, Shetta amesema kuwa mpaka sasa ana nyimbo 6 ambazo zimekamilika kitu, hivyo kimya ni maamuzi yake tu kwani muda wowote angeamua kuachia ngoma angefanya hivyo.
Loading...

No comments: