Waliosalimika vyeti feki wapewa ujumbe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 29, 2018

Waliosalimika vyeti feki wapewa ujumbe


Waliosalimika vyeti feki wapewa ujumbe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Mpoki Ulisubisya amewapongeza baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao walisalimika kwenye sakata la vyeti feki.


Ulisubisya ametoa kauli hiyo wakati akifunguza kongamano la Kisayansi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambalo liliwajumuisha jopo la wataalamu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini likilenga kutoa elimu juu ya kuzuia vifo vya kinamama.

“Nawapongeza wafanyakazi wote waliosalimika kwa vyeti feki, kwa sababu takwimu ambazo zilinifikia wizarani niliambiwa Muhimbili kulikuwa na watu wenye vyeti feki, sasa mkafanye kazi kama wataalamu wenye sifa.”

Akizungumzia kongamano hilo Mpoki amewataka watumishi wa Muhimbili kufahamu hospitali hiyo ni tegemeo kwa watanzania nchini hivyo hawana budi kuweka nadhiri kuwa kila mgonjwa anayefika hospitalini hapo anakuwa na uhakika wa kupona.

 “Sisi kwa umoja wetu tunaweza tukaamua kila anayekuja hospitali hapotezi maisha, tunaweza kwa kuweka dhamira kwa kila mmoja wetu katika dhana ya kutenda, na kufikiria, kwa hiyo lazima Muhimbili iangalie maeneo mengine ili kujifunza,” ameongeza Mpoki.
Loading...

No comments: