WATEJA WA TIGO SASA WANAWEZA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 29, 2018

WATEJA WA TIGO SASA WANAWEZA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed(wa katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini. (GePG)
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya(Kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini. (GePG)
Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto)  akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini. (GePG)Fanya malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama zaidi kwa zaidi ya idara 300 za serikali, mawakala na mamlaka za udhibiti kwa Tigo Pesa

29 Januari, 2018. Dar es Salaam.  Wateja wa Kampuni ya Tigo, sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

Akiongea katika uzinduzi wa GePG kwa mtandao wa Tigo yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na Mipango alisema kuwa ubunifu na juhudi za Serikali katika  kuanzisha mdumo huo wa Kieletronbiki wa Malipo Serikalini (GePG) umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi. Pia imeleta faida nyinginezo ikiwemo kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvuvaji na ubadhirifu pamoja na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali. na

Kupitia mfumo wa GePG Serikali pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali au kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufanya malipo ya ankara kwa urahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao. 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo na mkakati wetu,” alisema Hussein Sayed, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kifedha wa Tigo.

“Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya.

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Shirika la Kodi Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Mbuga za Wanyama (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300.

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala.


Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa kufuata hatua zifuatazo;.

1)      Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili
2)      Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali)
3)      Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka ipokee malipo
4)      Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa
5)      Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo

Kwa upande mwingine, wateja wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kukamilisha malipo, wateja wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika.

Tigo inawakaribisha wateja wake kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GepG) sasa.

Kuhusu Tigo

MIC Tanzania PLC ni kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma zinazohamasisha maisha ya kidigitali Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995. Kupitia bidhaa zake mbalimbali za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi; Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa Kiswahili, huduma ya Facebook bure kwa lugha ya Kiswahili, App ya TigoPesa, App ya Tigo Mobile pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki
.     
Tigo ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini na kwa miaka mitatu mfululizo, imekuwa kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini.

Tigo inajivunia zaidi ya watumiaji milioni 11 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja kwa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.  

Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na: 
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano
Simu: +255 713 123431            Barua pepe: Woinde.shisael@tigo.co.tz
Loading...

No comments: