WAZIRI LUKUVI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU MPYA NA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, November 1, 2018

WAZIRI LUKUVI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU MPYA NA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi ripoti Mapitio ya Muundo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sphia Kongela jana jijini Dodoma. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akifurahia jambo wakati alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk. Maulid Banyani wa kwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sophia Kongela wa pili kulia walipokuenda kujitambulisha ofisini kwake Dodoma, wengine kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Dk Angeline Mabula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Doroth Mwanyika. 
 
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Dk Sophia Kongela kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika nafasi hiyo, alipotembelea ofisi za Wizara ya Ardhi jijini Dodoma. 
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Naibu wake Dk Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Dk. Sophia Kongela wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu Dk. Maulid Banyani. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi Profesa John Lupala wakati akioneshwa ramani ya mji wa Serikali uliopo Dodoma.

Loading...

No comments: