Yondani, Kakolanya Waachwa na Kikosi Cha Yanga Kisa Hiki Hapa

Klabu ya Yanga imewaacha wachezaji wawili wa klabu ya Yanga Golikipa Beno Kakolanya na Beki wa klabu hiyo Kelvin Yondani katika kikosi cha Yanga kilichosafiri leo Alfajiri kwenda Mwanza baada ya kushindwa kuripoti kambini kama walivyoombwa na uongozi wa klabu hiyo.

Wachezaji hao walikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ' Taifa Stars' ambacho kilicheza mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON 2019) dhidi ya Lesotho siku ya Jumapili November 18 na kufungwa bao 1-0 na jana jioni waliwasili Tanzania na kikosi hicho.

Baada ya kuwasili majira ya saa 4:00 usiku, Gadiel Michael ndiye aliyeripoti kambini huku Kiungo Feisal Salum 'Fei toto' akiungana na kikosi hicho leo alfajiri ambacho kimeelekea Shinyanga kupitia Mwanza.

"Kweli wachezaji hao wamebaki Dar ila kesho wataondoka na kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera ambaye naye ameshindwa kusafiri baada kuwasili jana usiku akitokea kwao Congo," amesema Hafidh Saleh ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Siku ya Alhamisi ya November 22 katika dimba la CCM Kambarage Shinyanga.

Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea Bukoba, mkoani Kagera kwa  ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumapili ya November 25 Katika dimba la Kaitaba

Post a Comment

0 Comments