BAADA YA MAHAKAMA KUMREJESHA WAMBURA TFF, KARIA AJA NA TAMKO LA KIBABE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 2, 2018

BAADA YA MAHAKAMA KUMREJESHA WAMBURA TFF, KARIA AJA NA TAMKO LA KIBABE

TFF, KARIA ,TANZANIA

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema hatambui kurejeshwa madarakani kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Richard Wambura.

Karia ameeleza hayo baada ya Wambura kushinda kesi ambayo ilikuwa mahakamani iliyokuwa ikidai alifanya ubadhirifu wa fedha na TFF kumfungia kujihusisha na masuala ya soka.

Licha ya kushinda na mahakama kusema yuko huru kurejea kwenye nafasi yake, Karia amesema hatambui kurejea kwake akieleza jambo hilo lipo kwenye Kamati ya Maadili.

Baada ya Wambura kufungiwa soka, miezi kadhaa baadaye TFF ilitangaza kumchagua Athuman Nyamlan kuchukua nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.

TFF ilifikia hatua ya kumteua Nyamlan baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kwa miezi kadhaa na uoogozi wa juu kupitia Karia ukaamua kumteua Nyamlan kujaza nafasi ya Wambura.
Loading...

No comments: