BREAKING;Diamond Platnumz na Rayvanny wafungiwa Tanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, December 18, 2018

BREAKING;Diamond Platnumz na Rayvanny wafungiwa Tanzania


Diamond Platnumz na Rayvanny wamefungiwa kufanya onyesho lolote ndani na nje ya Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Baraza hilo limesema marufuku hiyo ya muda usiojulikana inaanza kutekelezwa leo.
Wasanii hao wawili walikuwa awali wametakiwa kuuondoa wimbo wao kwa jina 'Mwanza' kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini wimbo huo umeendelea kuwepo kwenye YouTube.
Aidha, wameendelea kuucheza kwenye matamasha.


"Baraza limefikia maamuzi ya kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018, chini ya uongozi wake Diamond Platnumz," taarifa ya Basata ambayo imetiwa saini na Onesmo Kayanda kwa niaba ya Katibu Mtendaji inasema.
"Pamoja na maelezo hayo, Baraza linatoa taarifa kuwa kibali cha Tamasha la Wasafi 2018 kimesitishwa kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini."
Loading...

No comments: