Mali za Yusuf Manji Ikiwemo Jengo la Quality Centre Hatarini Kufilisiwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, December 6, 2018

Mali za Yusuf Manji Ikiwemo Jengo la Quality Centre Hatarini Kufilisiwa


Mali za mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji zenye thamani ya mabilioni ya shilingi ziko hatarini kufilisiwa baada ya kuwekwa chini ya wadhibiti na wakabidhi wasii ili kulipa madeni makubwa yanayodaiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki na Kusini.

Mali hizo ni pamoja na jengo maarufu jijini Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Quality Centre.

Taarifa zilizotolewa jana na wafisili na wakabidhi wasii hao chini ya Kampuni ya Price Water House Coopers (PWC), ilisema kuanzia jana, Manji hataruhusiwa kumiliki mali hizo hadi atakapolipa madeni hayo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mameneja wanaosimamia kazi hiyo, David Tarimo na Nelson Msuya wameteuliwa na benki hiyo ili kukamilisha kazi ya ukusanyaji wa madeni na ikishindikana mali hizo zitapigwa mnada.
  
Jengo la Quality Centre lililojengwa zaidi ya miaka 10 iliyopita liko katika kiwanja Na.25 kandokando ya Barabara ya Nyerere (zamani Pugu Road) na katika miaka ya hivi karibuni, limekuwa kivutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na shughuli za kiuchumi zinazofanyika hapo.

Taarifa zinaeleza kuwa hata mali zilizomo ndani ya jengo hilo zinazomilikiwa na Quality Group Limited nazo zinashikiliwa.

Loading...

No comments: