Mtanzania Mbwana Samatta Kapewa Mkataba Mpya KRC Genk - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, December 24, 2018

Mtanzania Mbwana Samatta Kapewa Mkataba Mpya KRC GenkClub ya KRC Genk imetangaza good news kuhusiana na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye anaichezea club hiyo, KRC Genk imeonesha kuendelea kumuamini Mbwana Samatta na imeamua kumuongezea mkataba mpya staa huyo.

Samatta ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea KRC Genk, hivyo kutokana na mkataba wake wa awali kumalizika mwishoni mwa msimu 2018/2019, kutokana na kuongeza kwa mkataba huo atakuwa Luminus Arena hadi mwaka 2021.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mbwana Samatta alijiunga na KRC Genk January 2016 akitokea club ya TP Mazembe ya Congo, hadi sasa akiwa na KRC Genk amecheza jumla ya game 141, kafunga jumla ya magoli 55 ya mashindano yote na ametoa jumla ya assist 14 na kwa sasa ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli Ligi Kuu Ubelgiji akiwa kafunga magoli 12.
Loading...

No comments: