Papa Francis 'ahofia' makasisi ambao ni wapenzi wa jinsia moja - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, December 4, 2018

Papa Francis 'ahofia' makasisi ambao ni wapenzi wa jinsia moja


Pope Francis at the Vatican November 22, 2017.

Papa Francis ameonesha kusikitishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi
Papa Francis amesema mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi ni "jambo kubwa" na ambalo linampa "hofu". 
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini. Mahojiano hayo ni sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo. 
Papa amesema mahusiano ya jinsia moja ni jambo la "fasheni", na ametaka makasisi kutii viapo vyao vya utawa (kutojihusisha na mapenzi)

Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia limechapisha sehemu ya mahojiano hayo katika mtandao wake juzi Jumamosi. 
Papa Francis amesema kanisa katoliki linapaswa kuwa "imara" wakati wa kuchagua watu watakaokua makasisi. 
"Hili suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana," amesema Papa na kusisitiza kuwa wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi wahakikishe kuwa wanafunzi wao "wamekomaa kibinaadamu na kihisia" kabla ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho). 

"Kwa sababu hiyo, Kanisa linawataka watu wenye tabia hizo (wapenzi wa jinsia moja) wasikubaliwe katika maisha ya ukasisi."
Agizo hilo pia linawahusu wanawake ambao wanataka kuwa watawa wa kanisa hilo. 
"Katika jamii zetu, sasa inaonekana kuwa suala hili la mapenzi ya jinsia moja limekuwa fasheni. Mawazo kama hayo sasa yanaanza kupata ushawishi nadani ya kasnisa," amesema papa na kuongeza: "suala hili katu halina nafasi katika maisha ya watawa wetu."
Mwaka 2013, Papa alisisitiza juu ya msimamo wa kanisa hilo kuwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni dhambi. 
Kuhusu mahusiano binafsi ya Mungu na mtu mwenye kujihusisha na vitendo hivyo alijibu; "Kama mtu ni shoga na anataka ukaribu na Mungu na ana nia njema, mimi ni nani wa kuhukumu?" 
"Nguvu ya Utumishi", ni kitabu kilichotungwa na padre Fernando Prado,baada ya mahojiano ya saa nne na Papa kuhusu changamoto za kuwa kasisi. Kinatarajiwa kuchapishwa wiki ijayo.

CHANZO ; BBC SWAHILI
Loading...

No comments: