Rais Alazwa Kwaajili Kufanyiwa Uchungu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, December 13, 2018

Rais Alazwa Kwaajili Kufanyiwa UchunguRais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi amelazwa katika hospitali moja ya binafsi nchini Nairobi.

Kwa mujibu wa Daktari wake Dk. David Silverstein amesema kuwa ni jambo la kawaida kwa kiongozi huyo kulazwa na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na kwamba atakuwa hospitalini hapo kwa siku kadhaa.

Mapema mwezi Machi mwaka huu, Rais Moi alikwenda jijini Tel-Aviv nchini Israeli kwa ajili ya kuangalia goti lake ambalo lilikuwa linamsumbua ambapo serikali ilithibitisha kuwa matibabu yake yalikwenda sawa.

 Moi mwenye miaka 94, ambaye aliiongoza Kenya kwa miaka 24 kuanzia mwaka 1978 hadi alipostaafu mwaka 2002, alianza kusumbuliwa na goti Julai 30, 2006.

Januari 27, 2017 rais huyo wa zamani alifanyiwa upasuaji mdogo kwenye goti katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan huko Nairobi.
Loading...

No comments: